
Mama Monica Mutasingwa wa (kulia) ambaye alikuwa muumini wa zamani wa kanisa la Kakobe (Full Gospel Bible Felloship) na kufukuzwa katika kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Habari Maelezo juu ya kile alichokiita kuwa ni Unyanyasaji, Uonevu na uvunjwaji wa Haki za binadamu unaofanywa na Askofu Zakaria Kakobe zidi ya waumini wake akiwa kama kiongozi wa Dhehebu hilo kinyume na maandiko matakatifu na mahubiri yake kanisani hapo.Kushoto ni baba yake mzazi mzee Tara Sariyael.