Friday, July 16, 2010

KAKOBE MATATANI TENA........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Mama Monica Mutasingwa wa (kulia) ambaye alikuwa muumini wa zamani wa kanisa la Kakobe (Full Gospel Bible Felloship) na kufukuzwa katika kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Habari Maelezo juu ya kile alichokiita kuwa ni Unyanyasaji, Uonevu na uvunjwaji wa Haki za binadamu unaofanywa na Askofu Zakaria Kakobe zidi ya waumini wake akiwa kama kiongozi wa Dhehebu hilo kinyume na maandiko matakatifu na mahubiri yake kanisani hapo.Kushoto ni baba yake mzazi mzee Tara Sariyael.


Wednesday, July 14, 2010

ASYCUDA++, ASY-SCAN & IDF ONLINE

KWA HUDUMA ZA TANSAD PREPARATION, ASY-SCAN, IDF PREPARATION, ASYCUDA++ & VPN INSTALLATION, PAMOJA NA KUJIFUNZA, FIKA CLOCK TOWER SAMORA/UHURU JENGO LA DODOMA HOUSE KARIBU NA KAI SHOP, UTAKUTANA NA WATAALAMU WA ASYCUDA++, ASY-SCAN NA IDF ONLINE,

PIA KWA MATATIZO YOYOTE YA COMPUTER:- MAINTENANCE & REPAIR (SOFTWARE, HARDWARE, NETWORKING INSTALLATION AND STRONG ANTI-VIRUS INSTALLATION)

MAWASILIANO:-

0755-669634
joshy3vm@yahoo.com

WOZA 2010: MAMBO YA PWEZA HAYOO!!!!!!!!


HAPO PWEZA AKIWATABIRIA SPAIN KUWA NDIO MACHAMPION WA WOZA 2010 KWENYE ARDHI YETU (AFRICA) KWELI PWEZA HUYU NI KIBOKO JAMANI!!!!!

WOZA 2010: JAMAA ALITAKA KUGUSA KOMBE LA DUNIA DUH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!







KUMBE MAMBO HAYA SI BONGO TU, UKIACHILIA MBALI JAMAA ALIYETAKA KUMGUSA KAKA' PALE UWANJA WA TAIFA WAKATI BRAZIL IKIITIUNGUA TAIFA STARS, HUKO BONDENI KWA MADIBA JAMAA HUYO PICHANI ALIJITOSA ILI KULISHIKA TU KOMBE LA DUNIA, ALIFANIKIWA KUTIMIZA NIA YAKE!!!!!!!!!!!!!!

Wednesday, May 26, 2010

hepi besi dei ya kuzaliwa watoto wake mimi


tarehe kama ya leo mwaka uliopita namaanisha tar 26/05/2009 wanangu walizaliwa pale lugalo hosp, na leo ni mwaka sasa mapacha hawa wametimiza, hepi besi dei faraja & furaha wangu MUNGU awazidishie na awalinde siku zote za maisha yao

NIMESHAURIWA NITANGAZE NIA JIMBO LA KILOLO HUKU SI KUTEGANA JAMANI!!!!!


eti toka nimeanza kuvaa suti watu wengi wananipigia nitie "nia" kama wasemavyo wanasiasa wetu pale wanapotangaza kugombea majimboni, sipendi kutia nia maana mafans wa blog yangu watakuwa wanakosa mavituzzzzx since nitakuwa bizex sana na mambo ya cham, msijali jamani sitii nia, tupo pamoja "aluta continua"

UGONJWA WA KIBOFU CHA MKOJO


Mwalimu Marehemu Julias Kambarage Nyerere kuwa saint

The first Tanzanian president and father of the nation, the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere will be declared saint on June 1, 2010 in Namugongo, Uganda as part of the celebrations to mark this year's Martyrs' Day. Heads of states of African countries and Nyerere's widow Maria Gabriel Magige will attend.

President of Uganda, Yoweri Museveni supported the campaign to have Nyerere recognised as a saint. The campaign began in January 2006, when Rome accepted the request from Bishop Musoma of Northern Tanzania Diocese.

Meanwhile, preparations for the celebrations are in high gear. Fr. Dennis Ssebuggwawo, the shrine rector, said the programme at the Catholic Shrine will begin with a nine-day Novena (reciting of prayers) from May 26 to June 2. Ssebuggwawo said Moroto diocese will host this year's celebrations under the theme "I am with you always, yes to the end of the time (Mathew 28:20)".

Twenty-two Uganda martyrs were murdered at the Catholic shrines between 1885 and

Monday, May 24, 2010

hukumu ya liyumba mahakamani leo!!!!!

Hukumu ya kwenda gerezani na kutumikia kifuncho cha miaka miwili jela ndiyo adhabu anayoanza kuitumikia aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania BoT Amatus Liyumba, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo wakati akiwa kazini, hususana wakati wa ujenzi wa maghorofa pacha ya BOT jijini Dar.

Hata hivyo leo hii katika mahakama hiyo, mahakimu watatu wanaounda jopo la mahakimu linalosikiliza kesi hiyo, walitofautiana huku wawaili kati yao wakiwa na mtazamo mmoja wakati wa uandikaji na usomwaji wa hukumu yao.

Wawili hao ambao ni hakimu Benedict Mwingwa pamoja na Lameck Mlacha, waliandika na kusoma hukumu iliyofanana ambayo kimsingi ndiyo iliyomtia hatiani Liyumba na kumsababishia kupata adhabu hiyo.

Kwa upande wa Hakimu Mkasimongwa ambaya ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo hilo la mahakimu, ndiye aliyeandika hukumu yake tofauti hukumu ambayo ilionesha kumuachia huru mshatakiwa kwa kuwa hana hatia.

Lakini kutokana na nafasi kubwa na kuungwa mkono iliyoonekana na mahakimu wawili, ilisababisha mahakama hiyo kuichukua kiutekelezaji hukumu ya mahakimu hao Mlacha na Mwingwa na kumuhukumu Liyumba kifungo hicho.


Akisoma hukumu hiyo iliyomtia hatiani Liyumba, Hakimu Mlacha alisema kuwa ushahidi wa mashahidi nane wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, ndivyo vilivyopelekea mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.


Mlacha alisema kuwa, alisema kuwa Liyumba alisahini barua za mahidhinisho ya ufanyikaji wa mabadiliko ya ujenzi wa jengo la BoT, wakati hakiwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.

Aliongeza kuwa barua hizo zilikuwa na sahihi yake Liyumba jambo ambalo ni kinyume kwani ilitakiwa ziidhinishwe na bodi ya benki na si kurugenzi kama ambavyo alikuwa akifanya Liyumba.

Pia mahakama hiyo iliukataa ushahidi wa utetezi uliotolewa mahakamani hapo na Liyumba, ushahidi ambao ulidai kuwa mammlaka ya kusahini barua hizo, alipewa na aliyekuwa Gavana wa benki hiyo Daud Balali kwa njia ya mdomo.

Mlacha alisema kuwa mahakama imeingia mashaka juu ya kuamini hilo, kutokana na ukweli kuwa BoT ni taasisi ambayo kulingana na ukubwa wake na uzito wake hisingeweza kutoa maamuzi au kuumpa mtu madaraka makubwa pasipo kutumia maandishi hili kutunza kumbukumbu.


Aliongeza kuwa Mahakama hiyo inauchukulia ushahidi wa utetezi uliotoewa mahakamani hapo, si wa kweli kwani hata mmoja wa mashahidi wa upande wa mashtaka aliithibitishia mahakama hiyo kuwa maelekezo ya Gavana yalikuwa yakitoka kwa barua.


"Hata shahidi wa nne wa upande wa mashtaka bwana Michale Shirima, ambaye alikuwa mjumbe wa bodi ya benki, aliithibitishia mahakama hii kuwa maamuzi ya Gavana yalikuwa yakitolewa kwa maandishi na si kwa mdomo kama Liyumba alivyotuambia"alisema Mlacha.

Mbali na hilo, mahakama pia iliukataa ushahidi wa shahidi wa pili wa utetezi ambaye ni aliyekuwa Katibu wa Benki bwana Bosco Kimela, kwa kuita ushahidi huo kuwa ulikuwa wa kutungwa na mstakiwa pamoja na shahidi huyo.


Mlacha alisema kifungu namba 96 (1) cha Kanuni ya adhabu, kinasema kwamba iwapo mtu aliyeajiriwa katika taasisi ya umma, akielekeza kufanyika kwa jambo kinyume na sheria na taratibu za ofisi na hivyo kusababisha madhara kwa mtu mwingine, atakuwa ametenda kosa.

Aliongeza kuwa baada ya kupitia kwa makini kifungu hicho, mahakama imeona kuwa kosa alilotenda Liyumba lilikuwa ni kinyume na sheria na kwamba lilileta madhara kwakuwa gharama za ujenzi wa jengo hilo zilipanda kulinganishwa na zile zilizopangwa kwenye mkataba uliopitishwa na bodi hapo awali.


Kwa upande wa Wakili wa utetezi Majura Magafu, kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo aliiomba mahakama hiyo kupanga adhabu kwa kuangalia kifungu cha 38 (1) 16 ambacho kinairuhusu mahakam kutoa adhabu ya faini, ama kifungo cha nje kwa mashtakiwa.


“Muheshimiwa tunaiomba mahakama iweza kukiangalia kifungu hicho na kumpa mshatakiwa adhabu ya kulipa faini, au kifungo cha nje hasa ikizingatiwa umri wa mshtakiwa ni wa miaka 62 na vilevile anamaatatizo ya kiafya.

Magafua alidai kuwa mahakama izingatie kwamba Liyumba nategemewa na familia yake.

Lakini mambo yalikuwa tofauti wakati wa upangaji wa adhabu hiyo, ambapo Hakimu Mlacha na Mwingwa walipingana na maombi hayo ya magafu.

Pamoja na maombi hayo kwa mahakama, Hakimu Mlacha alitoa adhabu ya kifungo hicho baada ya kusema kuwa mshtakiwa hasingeweza kulipa faini hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna mapambano ya vitendo vya rushwa.

Kwa upande wa Hakimu Edson Mkasimongwa, alisoma huku yake aliyoiandaa ambayo ilipingana na hukumu ya awali, ambapo pia ilisomwa hili kutunza kumbukumbu za mahakama.

Mkasimongwa alisema kuwa upande wa mashataka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya Liyumba, hivyo anatakiwa awe huru kutokana na hilo.

Mkasimongwa alipingana na hoja ya kuwa mshtakiwa alisahini barua za kuhidhinisha kufanyika kwa mabadiliko wakati akiwa hana mamlaka hayo, kwasababu haikuwa na msingi.

Aliongeza kuwa kwa upande wa hilo, yeye haoni kama ni kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwani Liyumba kama mkuu wa kurugenzi iliyokuwa ikisimamia ujenzi huo alikuwa na na mamlaka ya kusahini barua hizo kama aliona kuwa hazikuwa na ubishani.

Hukumu hizo zilipomalizika kusomwa , Liyumba aliondoka mahakamani hapo huku akilindwa na askari kuelekea kwenye gari la magereza.

ZIMEBAKI SIKU 17 TU !!!!!!!!!!!

SIKU 17 TU ZIMESALIA, WAAFRIKA TUZIDI KUMWOMBA MUNGU AMANI ITAWALE NA MUNGU AMZIDISHIE SIKU MZEE WETU NELSON MANDELA ILI APATE KUONA NASI KOMBE HILI KUBWA LA DUNIA. AFRIKA PAMOJA!!!!

liyumba ala mvua mbili 2

hatimaye mahakama imemuhukumu liyumba kwenda jela miaka 2, habari kamili baadae

Wednesday, May 19, 2010

YANGA WACHACHAMAAA WAMTIMUA AMIR MAFTAH

HABARI AMBAZO TUMEZIPATA KUTOKA JANGWANI MAKAO MAKUU YA YANGA ZINASEMA KWAMBA YANGA WAMEMTIMUA MCHEZAJI WAO MAHIRI AMIR MAFTAH (pelle wa mwanza) KWA KOSA LA KUMPIGA KICHWA MCHEZAJI WA SIMBA WAKATI TIMU HIZO MBILI ZILIPOPAMBAMBANA UWANJA WA TAIFA, KATIKA KUTHIBITISHA HILO MWENYEKITI WA YANGA BW IMANI MAHUGIRA MADEGA ALITAMKA HILO WAKATI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI NA BAADHI YA WANACHAMA NA WAPENZI WA TIMU HIYO NA KWA MAANA HIYO SASA AMIR MAFTAHA YUPO HURU NA TIMU YOYOTE INAYOMUHITAJI IMCHUKUE, PIA AKIZUNGUMZIA JUU YA MRISHO NGASA NA NADIR HAROUB CANAVARO, MADEGA ALISEMA NGASA NI MCHEZAJI WETU (YANGA) BADO MPAKA 2012, NA HANA RUHUSA KUZUNGUMZA NA KLABU YOYOTE ILE, NA HATA KLABU YOYOTE HAIRUHUSIWI KUZUNGUMZA NA NGASSA KWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA FIFA, NA PIA AKIONGELEA KUHUSU CANAVARO, NAYE BADO NI MCHEZAJI WETU HALALI NA TUNAMKATABA NAYE HUKU AKIONYESHA MKATABA ULIOSAINIWA NA CANAVARO, HABARI ZAIDI TUTAPEANA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA

Wednesday, March 31, 2010

PICS MTINDO MMOJA!!!!!!!!!!!!

MY WIFE WAKE MIMI (ROSE)
BAADA YA KULA MINYAMA NYAMA MAMBO YA STIK MDOMONI

MY WIFE WAKE MIMI NA MY WATOTO WAKE MIMI, NAJUA KUNA WATU KAMA AKINA GRACE, JOAN MICK MUDDY SALVATORY, MGIMWA MLIKUWA NA HAMU SANA YA KUMWONA MY WIFE WAKE MIMI HUYO HAPO JAPO KUWA PICS HIZO NI ZA MWEZI JANUARY ILA SI VIBAYA MKIZIONA TU THEN NITAWALETEA UPDATED ONESSSSS

LEO NI MA PICSS TU KWENDA MBELE!!!!!!!!!

UNADHANI UNANIJUA MIMI? MIMI NDIO MY WIFE WAKE JOSHUA
RAHA KUWA MAMA JAMANI DUH
BUSU LA MAMA HILOOOOO MWAAAAAAAAAAAAA
"MTOTO HUYU ANA MAJASHO DUH "NADHANI NDIO ALIVYOKUWA ANASEMA MY WIFE WAKE MIMI HAPO TUKIWA KANISANI TUKISUBIRI UBATIZO WA WATOTO WETU
HAPA WALIKUWA NA MIEZI 5 TU MABINTI HAWA

Friday, March 26, 2010

HII HAIJATOKANA NA CHINA PRODUCTS JAMANI!!!!!!!!!!!!


HUYU DADA ANAISHI TABATA NA HAJAWAHI KUTUMIA CHINA PRODUCTS KAMA WENGI WANAVYOMUANDAMA NA KUMSAKAMA NA WENGINE KUMPIGA VIJEMBE KUWA "ATAJUTA KUWAFAHAMU WACHINA" UKWELI NI KWAMBA HAJAWAHI KUTUMIA MADAWA YA KICHINA NA AMESISITIZA KUWA TANGU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 12 MAUMBILE YAKE YALIANZA KUWA MAKUBWA SANA, LAKINI MWENYEWE ANASEMA WALA HAPATI SHIDA NA WANAOSEMA MAANA UKWLI ANAO MWENYEWE, KUTOKANA NA KERO ANAZOPATA BASI AKANIOMBA NIITOE HII KWENYE SATELITE ILI WADAU MJUE KUWA ILE NI GENUINE SIO CHINA PRODUCTS!!

Friday, February 12, 2010

matokeo kidato cha nne yametangazwa, ki ukweli si mazuri sana kiujumla ukitaka kujua kwa kiasi gani please gonga hapa http://www.necta.go.tz/html_csee209/olevel.htm

Friday, January 22, 2010

NO COMMENTS...............!!!



MY WIFE WAKE AKIMCHUNGULIA MTOTO, HUKU BABA WAWILI NAYE AKIANGALIA KWA TABASAMU BILA KUKWEPESHA MACHO, NO COMMENT KAKA, TUNASUBIRI MABINTI WAKUWE TUWATUME KWA SHOP,

MMMMMMH BABA WAWILI NAYE......!!!!!!


BABA WAWILI AKITETA JAMBO NA MAMA WATOTO WAKE, KULIA KWAKE NI SHEMEJI YAKE, NA WALIOBEBWA NI WANAWE WAWILI FURAHA & FARAJA!!!

HEPI BESI DEI BABA WAWILI...............!!!!!!!!!!


20 January ilikuwa ni birthday ya joshua (baba wawili) kama ilivyokuwa kawaida huwa kunakuwa na kiparty flani hv, lakini kutokana na 20 kuwa j5, familia ameandaa home party kesho jumamosi kwa marafiki na majirani wote pale nyumbani kwake tabata kuanzia saa 6 mchana lunch mpaka saa jioni hv, ukiwa rafiki, jirani, jamaa wa familia hii unakaribishwa kujumuika pamoja kwenye party hii!!!

CCM IMAJIFUNGUA MTOTO ANAITWA CCJ

WAKATI kukiwa na taarufa za baadhi ya vigogo wa CCM kujiengua, jana Msajili wa Vyama vya Siasa alipokea maombi ya usajili wa Chama Cha Jamii (CCJ), ambacho kinahusishwa na kumeguka kwa chama tawala.

Kuwasilishwa kwa maombi hayo kumekuja wakati hali ya hewa ndani ya CCM ikiwa imechafuka baada ya vita dhidi ya ufisadi kuonekana kuwagawanya vigogo wa chama hicho, huku hali visiwani Zanzibar ikizidi kuwagawa wanachama wa chama hicho tawala.

Wakati baadhi ya vigogo wa CCM wanaonekana kutoridhishwa na hali inayoendelea kwenye chama hicho tawala na kuhusishwa na mipango ya kuunda chama kipya, watu wawili jana walitinga ofisi za msajili wa vyama vya siasa kuwasilisha maombi ya usajili wa chama kipya.

"Ndio, leo walikuja kwangu watu wa Chama cha Jamii na nimepokea maombi yao. Kwa kifupi ni hivyo ukitaka zaidi njoo ofisini kwangu," alisema Msajili John Tendwa alipoulizwa kuhusu kuwasilishwa kwa maombi hayo na watu waliojitambulisha kuwa ni Richard Kiabo, ambaye anakuwa mwenyekiti wa muda na Renatus Muwadi, ambaye ni katibu mkuu wa muda.

Dira na lengo kuu la CCJ ni Ustawi na Hifadhi ya Jamii pamoja na demokrasia, kwa mujibu wa rasimu ya katiba ya chama hicho ambacho makao yake makuu yatakuwa jijini Dar es Salaam, huku ofisi ndogo zikiwa Zanzibar na Dodoma.

Kwa mujibu wa rasimu ya katiba ya CCJ bendera ya chama hicho itakuwa na rangi nne ambazo ni bluu, dhahabu, nyeusi na kijani, rangi ambazo zinapishana kidogo na za bendera ya taifa.

Rasimu hiyo, ambayo gazeti hili tayari limeipata, inafafanua kuwa rangi ya bluu ni ishara ya maji yanayounganisha pande mbili za Muungano yaani Zanzibar na Tanganyika, dhahabu, rasilimali za Tanzania, nyeusi ni watu na kijani ni kilimo, mazingira na uoto.

Imebainisha kuwa itikati ya CCJ ni demokrasia ya kijamii inayozingatia umoja wa taifa, utawala wa katiba na sheria, mgawanyo wa mamlaka ya dola, haki za binadamu, uhuru na ustawi wa jamii.

Aidha, misingi ya kiitikadi na nguzo za CCJ ni utawala wa dola na miiko ya uongozi ambapo imani yake kuu ni kwamba binadamu wote ni sawa, huzaliwa huru na Waafrika ni taifa moja. Pia kinaamini umoja wa Tanzania ni nguzo kuu ya umoja wa taifa la Waafrika na ni moja ya malengo makuu ya dola la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari za uhakika ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa viongozi hao wa muda wa CCJ wametangulizwa na baadhi ya vigogo kutoka ndani ya CCM ambao wanaandaa mikakati ya kukihama chama hicho katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Habari zinasema kuwa vigogo hao wa CCM, wakiwemo viongozi wa zamani na wabunge, wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kujadili mkakati huo na mpango wao wa awali ulikuwa ni kupambana na Rais Jakaya Kikwete ndani ya chama katika uchaguzi wa Oktoba.

Hata hivyo, habari hizo zinadai, ilionekana kuwa vigumu kumshinda Kikwete katika kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais kutokana na kusaliwa na muda mfupi wa kukampeni na ndipo walipoamua kusajili chama kipya.

Inasemakana kuwa baada ya kuvuja kwa mpango wa kuanzisha chama, vigogo hao walitaka kuingia kwenye moja ya vyama vya upinzani, lakini baada ya majadiliano ilibainika kuwa mpango huo unaweza kusababisha matatizo kama ilivyokuwa kwa NCCR Mageuzi.

NCCR, ambayo ilichomoza kwa nguvu na kujipatia wanachama wengi kiasi cha kuitikisa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, nusura isambaratike baada ya wanachama kuanza kumpinga Augustine Mrema aliyepewa uenyekiti na ugombea urais baada ya kujiengua CCM.

Habari zinasema kwamba tofauti na Mrema ambaye alitoka CCM akiwa peke yake, vigogo wa CCM watakuwa na kundi kubwa la vigogo wa CCM.

"Wanaweza kuwako zaidi ya wabunge 20 wa CCM, vilevile, kuna wabunge wa upinzani nao watakuwako katika kundi hilo. Kinachosubiriwa ni muda wa kufanya maamuzi hayo," alisema mtoa habari ambaye ameshiriki kila hatua ya kuanzisha chama hicho.

Habari za ukakika zinadai kuwa CCJ kimeratibiwa kwa karibu na vigogo wa CCM kwa kushirikiana na wanasheria makini.

"Chama hiki kimeanzishwa kutokana na maombi ya wanachama wa CCM, wanachama wa vyama vya upinzani na wananchi," alisema katibu wa CCJ, Muwadi.

"Ni mawazo ya wananchi, wafanyakazi, wastaafu, baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani na chama tawala cha CCM."

Hata hivyo, viongozi hawa wa muda watarajiwa kuwaachia madaraka vigogo hao wa CCM ambao wana ushawishi mkubwa kwa jamii mara watakapotangaza hatua ya kukihama chama tawala.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanatabiri kwamba kuanzishwa kwa CCJ kunaweza kuvuta vyama vingine vya upinzani kama NCCR-Mageuzi, Chadema na hata CUF kwa upande wa Bara na kushirikiana hivyo kutoa changamoto kubwa kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Vilevile, CCJ huenda kikachukua wabunge wengi wa sasa kutoka CCM ambao wanaweza kuangushwa katika kura za maoni, hivyo kikawa na nguvu zaidi.

Ni kwa mantiki hiyo pia wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona nguvu ya vyama vya upinzani vilivyopo sasa kupungua kutokana na uwezekano wa kupoteza wapenzi na wanachama kwa chama hiki kipya.

Vita ndani ya CCM imeonekana kuwa ni kubwa tangu kuibuka kwa kashfa ya Richmond iliyosababisha mgawanyiko mkubwa kuanzia kwa vigogo hadi wanachama wa CCM. Vita hiyo imekuwa ikipiganwa ndani ya chama, Bunge na nje, kiasi kwamba halmashauri kuu iliunda kamati ya watu watatu kujaribu kuondoa tofauti hizo.

Hata hivyo, habari zinasema kuwa kamati hiyo inaonekana kushindwa kuibuka na mapendekezo ya maridhiano yanayoweza kuridhisha pande zote mbili, hali ambayo imesababisha kila kundi kuanza mikakati yake kwa ajili ya Uchaguzi Kuu ujao.

CCM ilikuwa iitishe vikao vyake vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, lakini ilishindikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuingiliana kwa ratiba ya vikao hivyo na vile vya Baraza la Wawakilishi.

Hata hivyo, hali si nzuri visiwani Zanzibar ambako urafiki mpya wa Rais Amani Abeid Karume na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Seif Sharrif Hamad unaendelea kukomaa kiasi cha chama hicho kupendekeza mtoto huyo wa muasisi wa taifa la Zanzibar aongezewe muda.

Pendekezo hilo la CUF limeungwa mkono na wanachama wa CCM wanaoonekana kumuunga mkono Karume, huku wapinzani wake wake wakipinga maafikiano hayo na mpango wa kumuongezea muda kiongozi huyo wa SMZ.

Tayari mwakilishi wa CUF ameshawasilisha kwa katibu wa Baraza la Wawakilishi hoja yake binafsi ya kutaka marekebisho ya katiba ili Karume aongezewe muda kuhitimisha kazi aliyoianza ya kuondoa siasa za chuki na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi, ambao umeelezewa kuwa ndio chanzo cha machafuko visiwani humo.