Tuesday, December 15, 2009

JAMANI JAMANI DAR MVUA KIDOGO TU BALAA


HAYA NI MAENEO YA BUGURUNI BAADA YA MVUA KUNYESHA JANA, MADIMBWI KADHAA YALIJITOKEZA MITHILI YA MAZIWA KATIKATI YA BARABARA NA KWENYE BAADHI YA MITAA, HII NDIYO DAR YETU JAMANI

Tuesday, December 8, 2009

STARS LEO MSITUANGUSHE JAMANI


BAADA YA WENZETU WA NZANZIBAR JANA KUVUKA KWA KUWAVURUMUSHA NJE WAZAMBIA KWA MIKWAJU YA PENALT, LEO NI ZAMU YETU WABARA PALE TUTAKAPOPAMBANA NA ERITREA KWENYE MCHUANO WA ROBO FAINALI, NI WAZI KWAMBA ILI MIOYO YA WATANZANIA ITULIE NI LAZIMA KILIMANJARO STARS ISHINDE TU LEO, NAAMINI TUNAWEZA MAANA STARS INA KILA KITU, INA FULL SUPPORT INA WASHAMBULIAJI WENYE UCHU KAMA AKINA MRISHO NGASSA NA WENZAKE PALE NYUMA WAPO WA KUTOSHA WAKIONGOZWA NA AKINA SUED BASI BURUDANI TU, LAKINI USHINDI LAZIMA UPATIKANE LEO. KILA LA KHERI STARS HUKO KENYA

KATUNI YA LEO..........

Monday, December 7, 2009

GOOD NEWZZZZZZZZZZZZZ


TAARIFA ZILIZOTUFIKIA ZINATANABAISHA KUWA KIKOSI CHA IVORY COAST KITAWEKA KAMBI BONGO KWA AJILI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2010 HUKO BONDENI KWA MADIBA, HABARI ZILIZOTUFIKIA ZINASEMA KUWA JAMAA WAMEVUTIWA NA UWANJA NA PIA HALI YA HEWA YA HAPA AMBAYO HAITOFAUTIANI SANA NA WAO, HABARI ZAIDI ZITAWAJIA PUNDE TUTAKAPOZIPATA

MGOMO TABATA!!!

HABARI TULIZOZIPATA PUNDE TOKA TABATA NI KWAMBA ABIRIA WA KUTOKA TABATA SEGEREA, LIWITI, CHANG'OMBE NA MAENEO YOTE YA TABATA KWA UJUMLA LEO WPO KATIKA ADHA KUBWA YA USAFIRI KUFUATIA DALALA ZINAZOHUDUMIA NJIA HIYO KUGOMA KUPINGA OPERESHENI INAYOENDESHWA NA MAJEMBE AUCTION MART YA KUPIGWA FAINI KATI YA TSH 200000 NA 250000 KWA DALADALA LITAKALOPATIKANA NA MAPUNGUFU, HIVYO MADEREVA NA MAKINDAKTA WALIPANGA KUGOMA NA KUFANYA MKUTANO WAO ENEO LA LIWITI SHULENI ILI KUZUNGUMZIA HATMA YAO. HABARI KAMILI NI KADRI TUTAKAPOZIPATA KUTOKA KWA MWANAHABARI WETU ALIYEPO KULE

Friday, December 4, 2009

KILA LA KHERI KILIMANJARO STARS


KWA VYOVYOTE VILE STARS INATAKIWA KUSHINDA MECHI YA LEO ILI IJIWEKE KATIKA MAZINGIRA MAZURI YA KUINGIA ROBO FAINALI, UKIZINGATIA MATOKEO YA MWISHO YA UGANDA AMBAPO WALIWASHINDA BURUNDI 2-0, KAMA WALIVYOWASHINDA KILIMANJARO STARS KWA IDADI HIYO HIYO YA MAGOLI NA KUFIKISHA POINTI 6, KWA MSIMAMO HADI SASA UNAONYESHA KUWA UGANDA AMBAO NDIO WATETEZI WA KOMBE HILO WANAONGOZA KWENYE KUNDI LAO WAKIFUATIWA NA ZANZIBAR HEROS YENYE POINTI 3 SAWA NA TZ BARA LAKINI WANATOFAUTIANA KWA IDADI YA MAGOLI, ZANZIBAR WAKIWA WAMEFUNGA MAGORI 4 NA KUFUNGWA 1 NA NDUGU ZAO WA BARA WAKIWA WAMEFUNGA GOLI 1 NA KUFUNGWA 2, NA WANAOSHIKA MKIA NI BURUNDI BAADA YA KUPOTEZA MECHI ZOTE MBILI, KILA LA KHERI KILLIMANJARO STARS

KESI YA BABU SEYA ILIVYOLIPUKA JANA MAHAKAMANI


MAWAKILI wanaomtetea mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini, Nguza Viking maarufu ‘Babu Seya’ na wanawe watatu, wameiomba mahakama kuwaachia huru warufani kwa kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kupangwa.
Sambamba na hilo, mawakili hao; Mabere Marando na Hamidu Mbwezeleni, walieleza kuwa tangu waanze kazi ya uwakili miaka 30 iliyopita, hawajawahi kuona hukumu ya ovyo kama hiyo.
Mawakili hao walieleza hayo jana mbele mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Nataria Kimaro, walipokuwa wakiwasilisha sababu za kupinga rufaa ya Mahakama Kuu iliyolewa na Jaji Msaafu, Thimas Mihato na hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Addy Lyamuya ambao wote walitia hatiani kwa makosa ya kubaka.
Majaji wengine wanaounda jopo hilo ni Salum Massati na Mbarouk Mbarouk.
“Waheshimiwa majaji, sisi tunasema jaji na hakimu huyo walikosea kisheria, kwani sheria inaitaka mahakama kabla haijaanza kuchukua ushahidi wa mtoto ni lazima ijiridhishe mtoto huyo ana akili timamu na anaelewa maana ya kiapo na kisha irekodi hayo kwenye jalada la kesi, lakini Hakimu Lyamuya hakufanya hivyo.
“Mashahidi 10 ambao ni watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 6-8 ambapo upande wa mashitaka ulidai walibakwa na kulawitiwa na warufani, walipofika Mahakama ya Kisutu kutoa ushahidi wao hawakuhojiwa na wala mahakama haikujiridhisha kama wana akili timamu, kwa sababu hiyo tunasema kwamba ushahidi wa watoto hao ni batili na tunaliomba jopo lenu lisiukubali,” alidai Marando.
Marando alidai kuwa wakati akitoa hukumu hiyo, Hakimu Lyamuya aliandika maoni yake binafsi ambayo yanapishana na mashahidi wa upande wa utetezi, kitu ambacho kinapingana na sheria za nchi.
“Katika hukumu hiyo utaona wazi hakimu anabishana na shahidi baada ya kumbishia shahidi huyo kwamba si Mzaramo, wakati shahidi huyo aliiambia mahakama mama yake ni Mzaramo na baba yake ni Mkongo... haya ni mambo madogo, lakini yanaonyesha ni jinsi gani hakimu alivyopuuza ushahidi wa upande wa utetezi,” alieleza na kuongeza:
“Waheshimiwa majaji sijawahi kuona hukumu kama hii kwa miaka 30 tangu nianze kazi ya uwakili, kwani sote tunachojua maoni ya hakimu katika hukumu yanaandikwa pembeni, lakini katika hukumu hii hakimu ameweka maoni yake,” alidai Marando na kusababisha watu kuangua vicheko.
Akimuelezea mrufani Papi Kocha, alidai kuwa mrufani huyo alimweleza katika kipindi hicho alikuwa mikoani kwa ziara za kikazi, lakini hakimu Lyamuya katika hukumu yake akaweka mawazo yake kwa kusema hata kama alikuwa safari anaweza kutenda makosa hayo.
“Lakini majaji katika rufaa ya Mahakama Kuu hakuna ushahidi uliotolewa unaoonyesha warufani walibaka... hayo yalikuwa ni mawazo ya hakimu kwamba lazima Babu Seya na watoto wake waende gerezani, narudia tena sijawahi kuona hakimu wa aina hii na hukumu ya aina hii ambayo hakimu aliamua kuweka maoni yake binafsi.
“Ni wajibu wa mahakama kutafakari ushahidi wa utetezi hata kama hauna uzito, sasa huyu Lyamuya katika hukumu yake amewataja mashahidi wa utetezi waliokuja kutoa ushahidi bila kueleza mashahidi kwa mapana walieleza nini,” alidai.
Aidha, alidai mmoja wa mashahidi wa upande wa upande wa mashitaka ambaye hakuapishwa, alidai shahidi huyo alifundishwa kusema uongo wa dhahiri kwani mtoto aliiambia mahakama walikuwa wakifundishwa Kiingereza na aliyekuwa mshitakiwa wa tano ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye aliachiliwa huru.
“Ushahidi wake alidai Babu Seya alimbaka, lakini hakuna rekodi yoyote inayoonyesha shahidi huyo alimtaja. Shahidi huyo alitaja majina ya vijana waliomkamata ni Cheupe na Sembe na katika warufani hao hakuna mrufani mwenye majina hayo na upande wa mashitaka wala hawakuwaleta mahakamani watu hao, ili wawe mashahidi,” alidai Marando.
Akiendelea kuuchambua ushahidi huo, alidai kuwa ushahidi huo unaonyesha kuwa mtoto huyo alikuwa akibakwa hata siku ambazo si za shule na kutoa mfano kuwa Oktoba 11, mwaka 2004 ilikuwa Jumamosi na tayari Babu Seya alikuwa ameishakamatwa, lakini shahidi huyo alieleza kuwa siku hiyo alikuwa amebakwa.
Akichambua kwa ujumla ushahidi wa watoto hao, alidai kuwa hakuna shahidi wa upande wa mashitaka aliyeiambia mahakama kuwa makosa hayo yalitendekea Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba na Oktoba isipokuwa hati ya mashitaka inasomeka kwamba makosa yote yalitendeka kati ya Septemba na Oktoba, lakini juaji na hakimu huyo wakaridhia.
Aidha, alidai mmoja wa watoto hao alidai kubakwa hadi kutoka damu, lakini taarifa ya daktari iyowasilishwa mahakamani hapo ilionyesha kuwa mtoto huyo ni bikira na wala haonyeshi aliwahi kubikiriwa wala kuingiliwa kinyume na maumbile.
Pamoja na hayo, alihoji kilichofanya upande wa mashitaka kuficha ripoti ya daktari aliyewafanyia uchunguzi watoto hao wanaodaiwa walibakwa na kushindwa kuleta mashahidi ambao ni wanamuziki wa bendi ya Achigo, mama wa Babu Seya na mke wa Babu Seya kwa sababu waliona mashahidi hao wangewaumbua.
“Kesi hii ni ngumu kwetu sote na kama mahakama na sisi tunaona warufani walifanya haya makosa tuwalaani ila mimi Marando nasema nimejiridhisha hawajafanya hayo makosa.
“Hivi tujiulize, kibaiolojia kweli inawezekana mtoto wa miaka sita abakwe na wanaume hawa (warufani) nyuma na mbele halafu mtoto huyo aweze kutembea? Haiingii akilini hata kidogo, nasema kesi hii ni ya kutunga, kwani hata mwanamke mwenye umri wa utu uzima akifanyiwa unyama huo hawezi kutembea,” alidai Marando.
Akijibu hoja za mrufani, wakili Mkuu wa Serikali Justus Mulokozi, alidai kitendo cha shahidi kushindwa kumtambua mshitakiwa mahakamani si sababu inayosababisha ushahidi wa shahidi huyo kuonekana hauna thamani, jibu lililosababisha umati wa watu kuangua vicheko.
Mulokozi alidai pia mahakama ikiamini upande mmoja, hailazimiki kuangalia upande mwingine, hoja ambayo ilipingwa na Marando ambaye alidai kuwa hoja hiyo haikupaswa kutolewa na wakili mwandamizi kama Mulokozi kwani hoja hiyo inatofautiana na sheria za nchi na kauli ya wakili huyo wa serikali imedhihirisha ni kweli Lyamuya aliegemea ushahidi wa upande wa mashitaka.
Jaji Kimaro alisema jopo hilo tayari imeishamaliza kusikiliza rufaa hiyo na akasema jopo lake litatoa taarifa ya hukumu.
Mbali na Babu Seya, warufani wengine ni Papii Kocha Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

Thursday, December 3, 2009

mambo yetu yaleeeeeeee


MI CHICHEMI KITU, KAZI KWENU WADAU

NEWZ KUTOKA KWA PILATO

NEWZ ZINATABAISHA KUWA HUKO MAHAKAMANI MAMBO BADO KABISAAAAAA RUFANI YA BABU SEYA INAPIGWA DANADANA, TUTAENDELEA KUWAPASHA KADRI HABARI ZITAKAPOTUFIKIA

KWELI NYERERE ANGERUDI................


CHAPA HAOOOOOOOOOOOOO

SIMA INTERNET CAFEEEEEE...........

hii ni internet cafe inapatikana pale tabata opposite na st marys teachers college, high speed connection, fast web oppening na pia fast download, kutana na dada mahiri katika ku-design cards, proposal, typing na kila unachohitaji utakipata pale, SIMA internet cafe pia wanajishughulisha na maintanace (software and hardware) fika pale upate huduma murua kabisa na za uhakika:

kwa mawasiliano

DIRECTOR:-0756-306585, 0655306585

I.T MANAGER:- 0755669634

SECRETATY:-0714-793764, 0764861484

WOTE MNAKARIBISHWAAAAAAAAAAAAAAA

TRL HAKUKALIKI.......................!!!!!


JESHI la Polisi jana lilimnusuru mkurugenzi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), Hundi Chaudhary na menejimenti yake baada ya wafanyakazi kutaka kuwaondoa ofisini kwa nguvu.

Pamoja na kushindikana kwa jaribio hilo, wafanyakazi wa TRL wameamuru treni ya abiria, ambayo imetoka Dar es salaam juzi kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa, isiendelee na safari mara itakapofika Itigi ambako wametaka abiria wote washushwe.

Hasira za wafanyakazi hao, ambao wamekuwa wakimpinga kwa nguvu zote mwekezaji kwenye kampuni hiyo kubwa ya usafiri nchini, zimeongezeka kutokana na kutolipwa mishahara yao ya mwezi Novemba na hasa baada ya menejimenti kuwaambia kuwa haina fedha za kuwalipa mishahara.

Jaribio la kumwondoa mkurugenzi huyo lilifanywa baada ya wafanyakazi kufanikiwa kumwondoa msimamizi wa karakana ya kampuni hiyo iliyo Dar es salaam na kumtaka asionekana tena ofisini.

Kamanda wa poli kitengo cha Reli, Ruth Makelemo alisema baada ya tukio hilo kuwa wafanyakazi hao na uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) hawana mamlaka ya kuifukuza menejimenti ya TRL nchini.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkurugenzi huyo wa TRL, Chaudhary jijini Dar es Salaam.

“Mimi siwezi kuruhusu wafanyakazi kuwaondoa hawa jamaa ofisini kwa sababu hawana kibali cha kufanya hivyo. Nitawalinda mpaka dakika za mwisho pamoja na mali zao,” alisema Makalemo.

"Hali si shwari hapo nje wafanyakazi wamefunga barabara; hakuna hata pa kupita, je nikiruhusu waondoke kisha ikatokea mauaji hapo nje, nitajibu nini mbele ya viongozi wangu; wakitaka walete kibali kwanza vinginevyo hapa hatoki mtu.”

Msimamo wa ofisa huyo wa polisi ulizidisha hasira za wafanyakazi hao ambao baadaye walilazimika kugoma kufanya kazi na kusitisha huduma zote za treni hiyo hadi watakapopata mishahara yao.

“Kwa kuwa polisi mmeamua kutuzuia kumwondoa mwekezaji, sisi tunasitisha huduma zote za reli mpaka hapo tutakapolipwa haki yetu na pia hatutarudi kazini mpaka Wahindi waondoke,” alisema mmoja wa wafanyakazi aliyekuwa mstari wa mbele.

Baadaye wafanyakazi hao waliwaamuru wafanyakazi wa kitengo cha kuongoza safari za treni kupiga simu kwenye vituo vyote vya reli ili waizuie treli ya abiria iliyokuwa imeondoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya bara jana.

Na kiongozi huyo wa kitengo cha safari za treni ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisikika akizungumza kwa simu akisema: “Hapa Dar es Salaam hali si shwari. Wafanyakazi wameamuru treni ya abiria ikifika Itigi isimame na isiendelee na safari zake mpaka hapo itakapo tangazwa tena.”

Treni hiyo ya abiria iliondoka Dodoma jana saa 2:30 asubuhi kuelekea mikoa ya Mwanza, Tabora, Kigoma na Shinyanga lakini mpaka taarifa hiyo inatolewa jana mchana ilikuwa imefika Manyoni, lakini wakataka ishushe abiri Itigi.

Mkurugenzi mkuu wa TRL, Hundi Chaudhary hakutaka kuzungumzia lolote kuhusu jaribio hilo la wafanyakazi.

“Jamani ningependa mnipe nafasi kidogo nipumzike. Kichwa changu kimechoka sana; siwezi kuzungumza chochote leo,” alisema Chaudhary.

Katibu mkuu wa TRAWU Sylvester Rwegasira alisema chama chake hakikushiriki kumwondoa mwekezaji huyo na badala yake kilikuwa kinafanya naye mazungumzo ili aondoke mapema kabla ya jazba za wafanyakazi hao hazijakithiri.

TRL ni kampuni iliyoundwa kwa ubia baina ya serikali na kampuni ya Rites ya India, ambayo ilishinda zabuni ya kuendesha huduma hiyo nyeti ya usafiri wa reli nchini. Rites imesaini mkataba wa miaka 25 na serikali, ambayo hata hivyo inaonekana kusita kuvunja mkataba ikidai italazimika kulipa fidia kubwa.

Mkataba wa serikali na Rites, ambayo inamiliki asilimia 51 ya hisa, ulisainiwa Oktoba mosi Mwaka 2007.

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA...............!!!!!!


SI KILA MAGHOROFA LAZIMA YAJENGWE KWA TOFALI, CEMENT NA HATA ALUMINIUM, CHECK NYUMBA HII YA MZEE KIKOFU AMBAYE YEYE YUPO CONFOTABO NA MAISHA YANASONGA TU,

HEBU FIKIRIA KAMA KAMJENGO HAKO HAPO NDIO KANGEKUWA EIZA B.O.T OR NDIYO MASKANI YA J.K NAMAANISHA IKULU, THEN USIKU TUNAWASHA KIKOROBOI WENGINE WAITA KIBATARI LAKINI NDIO HICHO HICHO TU, IMAGINE HAKUNA SIMU USAFRIRI UWE NI BAISKELI ZA MITI, NAJUA UMEANZA KUPATA PICHA SASA, MAISHA YANGEKUWAJE HAPO........................................

Wednesday, December 2, 2009

DAAAH JAMAA ALIKAMUA MPAKA DEGREE!!!


SEMAYONGA ERENEST AKABIDHIWA SHAHADA YA KWANZA, JAMAA NI MFUNGWA WA GEREZA LA UKONGA

WABAYA WA MAXIMO VICHWA CHINI STARS 1 - ZNZ 0

NANI KAKWAMBIA MAXIMO KIWANGO CHAKE KIMEFIKA MWISHO? WATU VICHWA CHINI BAADA YA MRISHO KHALFAN NGASSA KUTUMBUKIZA MPIRA KIMIANI KWA SHUTI KALI SANA. HII ILIKUWA JANA KULE KENYA KWENYE MASHINDANO YA CHALENGE

STARS OYEEEEEEEEEEEE.........!!!!!!!!!!!!!!!

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZZZZZZ!!!!!!!

mzee wa mipasho(fmeridian) wachuana kwa kasi na mzee wa tax mud kaupta VPN ya hooo........ lakini tulivyomfata hooo atupe ukweli yeye alitupa jibu moja tu "wote tomcat) wote hatujui ni nini maana yake tutaendelea kuwaletea maendeleo ya bifu hili kadri tutakavyopata newz

JAMANI JAMANI..................!!!!!!!



nilikuwa najiuliza kuhusu hizi pics ambazo huwa zinatatanisha watu, lakini sasa nimepata ukweli kumbe huyo sokwe demu ni VPN ya huyo komandoo aliyesimama ki-ukakamavu, nasikia connection ni mwanzo mwisho kama dereva wa guta